Rais wa Korea kusini Park Geun
Hye amemkosoa nahodha na wafanyikazi wa Feri ya abiria iliozama kwa
kuikimbia feri hiyo na hivyobasi kufananisha vitendo vyao na mauaji.
Matamshi ya rais Park yanafuatia uchapishaji wa
mawasiliano kati ya feri hiyo na waokozi, yaliobaini kwamba kulikuwa na
hali ya wasiwasi mbali na kutokuwepo mpangilio wa uokozi.
Idadi ya watu waliofariki
imeongezeka na kufikia 64 huku watu 238 wakiwa hawajulikani waliko,wengi
wao wakiwa wanafunzi wa shule.
Wapiga mbizi wanaendelea na juhudi za kutafuta
mili ya watu waliozama na feri hiyo huku wakijitahidi kuingia ndani ya
feri yenyewe.
Habari zilizotangazwa kuhusu mawasiliano ya
mwisho kati ya wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea Kusini na maafisa wa
kudumisha usalama baharini zinaonyesha kuwa kulitokea hali ya wasiwasi
kabla ya mkasa huo, ambayo huenda ilichangia pakubwa vifo vya abiria
wengi katika feri hiyo.
Taarifa hiyo mpya ilitolewa Jumapili alasiri
wakati ambapo imethibitishwa kuwa maiti 62 zimepatikana kwenye mabaki ya
feri hiyo, na kufanya idadi ya watu waliothibitishwa kufariki kufikia
58. Zaidi ya watu 240 hawajulikani waliko hivi sasa.
Jamii za watu ambao hawakuwa wamepatikana
walifanya maombi ya Pasaka Jumapili katika chumba cha kufanyia mazoezi
katika eneo la Jindo, ambako mamia ya watu wamekusanyika tangu feri hiyo
kupinduka wakisubiri habari kuwahusu wapendwa wao.
Mama mmoja alisema kuwa watoto waliofariki walikuwa wakitunzwa vizuri.
"Naamini watoto hao wako mbinguni ," mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea kuzisaidia
familia za walioathirika, alisema kuwa jamaa za watu wasiojulikana
waliko wanapaswa kusikia kilichotokea kwa njia moja au nyingine.
"ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata miili yao
haraka iwezekanavyo. Na iwapo kutatokea muujiza basi turejeshewe watoto
hao upesi pia, alisema mfanyakazi huyo wa kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo walikuwa
wanafunzi wa shule ya upili waliokuwa wakienda kwenye mojawapo wa kisiwa
kubarizi. Hadi kufikia sasa kumekuwa kungali kuna ubishi mkubwa iwapo
nahodha mwenyewe alikuwa ameshikilia sukani.
COPY PASTE from BBC
No comments:
Post a Comment