Saturday, March 22, 2014

AUSTRALIA: KUNA MATUMAINI MAKUBWA YA KUIPATA NDEGE YA MALASIA MH370

 
Waziri Mkuu wa Australia amesema kuwa kuna matumaini makubwa ya kupata mabaki ya ndege ya Malasia MH370 baada ya kusemekana kuwa kuna mabaki yameonekana baharini katika eneo walilokuwa wakiitafuta ndege hiyo. 

Hii huenda ikaondoa utata uliotawala kuhusu chanzo cha ndege hiyo kupotea na jumla ya watu 239 ikitokea nchini Malasia kuelekea nchini China.
Kuna wanaosema ilitekwa na wengine kuihusisha na hujuma ya marubani na baadhi kusema kuwa huenda ilijiendesha yenyewe umbali mrefu angani na kuishiwa mafuta kisha kuangukia mahali kusikojulikana.

No comments:

Zilizosomwa zaidi