WANNE WATIWA MIKONONI MWA POLISI KWA KOSA LA KULETA VURUGU MKUTANO WA CHADEMA-KIGOMA
Jeshi
la Polisi wilayani Kibondo mkoani Kigoma, limewakamata watu wanne kwa kosa la kutaka
kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa uliofanyika hapo jana katika kata ya Mabamba wilayani Kibondo Imeriptiwa kuwa watu hao walikuwa na mabango
yenye maneno yanayoonesha kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ya
kuwavua madaraka Zitto Kabwe na wenzake, lakini hata hivyo wameelekezwa
sehemu ya kukaa ili mabango yao yaweze kusomwa vizuri na Dk Slaa,
wamekaidi malelekezo hayo ambapo imebidi Dk Slaa aliagize jeshi la
Polisi kuwakamata watu hao kwani mkutano huo ni kwa mujibu wa sheria
Watu hao ambao majina yao hayakujilikana papo hapo wamepelekwa kituo
cha Polisi na Dk Slaa amemuagiza Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kibondo
kufuatilia kesi hiyo kwa ukaribu. Chanzo: REDIO KWIZERA
No comments:
Post a Comment