Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya
Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi,
David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili
Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba
majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa
maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.
Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika
Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika
mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa
baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga
Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi
nyingine iliyotengwa ni Burundi.
Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili
mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe
nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika
nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda
Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta
(Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi
ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment