Wednesday, October 16, 2013

SASA BAKWATA LAMALIZA MGOGORO WILAYA YA ARUMERU

DSCF0849Kushoto ni Mjumbe wa baraza la mashehe wilaya ya Arumeru, Haruna Hussein Lotta,pembeni ni viongozi wa zamani wakikabidhiana rasmi ofisi mara baada ya BARAZA kuu  la waislamu Tanzania (BAKWATA) kutatua mgogoro uliokuwepo kati  yao na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Arumeru na katibu  wa wilaya wa baraza hilo baada ya kusimamishwa nafasi zao za uongozi kwa kipindi cha miezi  saba.
DSCF0851Wajumbe wakifatilia kwa makini
DSCF0850
DSCF0852
Ndani ya kikao na wajumbe wa mkutano hali ilikuwa hivi
BARAZA kuu  la waislamu Tanzania (BAKWATA) limetatua mgogoro uliokuwepo kati  yao na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Arumeru na katibu  wa wilaya wa baraza hilo baada ya kusimamishwa nafasi zao za uongozi kwa kipindi cha miezi  saba.
 
Kaimu katibu  wa (BAKWATA) mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud alisema kuwa bazara  hilo limefikia hatua ya kuwarudisha viongozi hao kwenye nafasi zao baada ya kusimamishwa katika nafasi hizo kutokana na   ukwiukaji wa sheria walioufanya wakiwa madarakani kinyume cha sheria cha baraza hilo.
 
Alisema kuwa, baada ya baraza kuu kukaa na kufanya  vikao vyake , walipitia barua mbalimbali zilizoandikwa na viongozi hao za kuomba kurudi katika nafasi  hizo huku wakikiri kutorudia tena makosa waliyofanya ndipo baraza hilo lilipopitia na kuwarudisha tena katika  nafasi.
 
‘Sisi dini yetu inaturuhusu kusamehe na kuwasikiliza watu mbalimbali katika shida zao ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali iliyopo katika misikiti yetu lengo likiwa ni kuhakikisha kila mmoja wetu anaishi kwa amani  na kuondoa tofauti miongoni mwa waumini wetu kwani ndio lengo letu la kuleta amani kwa waumini na viongozi wetu kwa ujumla’alisema Kaimu katibu huyo.
 
Masoud aliwataka viongozi  hao pamoja na mashehe mbalimbali kuhakikisha wanahubiri amani katika maeneo yao sambamba na kuondoa migogoro iliyopo miongoni  mwao na hatimaye kuweza kuishi kwa amani na upendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.
 
Naye Mjumbe wa baraza la mashehe wilaya ya Arumeru, Haruna Hussein Lotta alisema kuwa, aliwataka viongozi mbalimbali wa dini hiyo kuacha   majungu na  unafiki badala  kwani kwa kufanya hivyo ndio wanazidi kuliharibu baraza hilo badala ya kulijenga.
 
Haruna  alisema kuwa,waislamu wengi sasa hivi wameishia kukaa na kupiga majungu na kusengenyana hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta mpasuko ndani ya baraza la bakwata wilaya ya Arumeru.
 
Aliongeza kuwa, endapo viongozi wa  dini hiyo pamoja na waumini hawataepuka masengenyo na majungu katika baraza hilo wataendelea kuwa na migogoro ambayo haitaisha, hivyo kuwataka kukaa na kuacha tofauti zao kwa muda huu ambao viongozi wamerudishwa katika nafasi zao na hivyo kulijenga baraza hilo ili lidumu na kuwa na amani toafuti na ilivyokuwa hapo awali.
 
Aidha waliorudishwa katika nafasi zao ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru ,Jumanne Zuberi na katibu wa wilaya Ramadhani Kumallah ambapo aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ya Mwenyekiti ni Yahaya Hajji na Katibu alikuwa Yahaya Mwengellah.

No comments:

Zilizosomwa zaidi