Thursday, October 31, 2013

KUELEKEA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE,IDADI KAMILI YA WATAHINIWA HII HAPA.......

Mitihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013 inatarajiwa kufanyika nchini kote kwa muda wa takribani siku 18 kuanzia tarehe 04-21
Novemba, 2013. Mitihani hiyo imetanguliwa na mitihani ya vitendo ya somo la ‘Food and Nutrition’ iliyofanyika tarehe 7- 24 Oktoba, 2013.
Jumla ya watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani ni 427,906 ambapo kati yao 367,399 ni watahiniwa wa shule na 60,507 ni watahiniwa wa Kujitegemea.
Idadi hiyo ya watahiniwa wote walioandikishwa mwaka 2013 ni pungufu ya watahiniwa53,508 sawa na asilimia 11.1 ikilinganishwa na watahiniwa 481,414 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka 2012. 
Watahiniwa wa shule (School Candidates):
Kati ya watahiniwa wa shule 367,399 walioandikishwa, wavulana ni 198,257 sawa na asilimia 53.96 na wasichana 169,142 sawa na asilimia  46.04. Watahiniwa hao wa shule wa mwaka 2013 ni pungufu ya Watahiniwa 15,195 sawa na asilimia 3.68 ikilinganishwa na watahiniwa wa shule 412, 594 wa mwaka 2012. Aidha, kati ya watahiniwa hao, watahiniwa 39 ni wasioona na watahiniwa 305 ni wenye uono ambao huhitaji maandishi
makubwa. 
Watahiniwa wa Kujitegemea (Private Candidates):
Kati ya watahiniwa wa kujitegemea 60,507 walioandikishwa wanaume ni 30,456 sawa na asilimia 50.33 na wanawake 30,051 sawa na asilimia 49.67. Watahiniwa wa Kujitegenea walioandikishwa mwaka 2013 ni pungufu ya Watahiniwa 8,313 sawa na upungufu wa asilimia 12.1 ikilinganishwa na watahiniwa 68,820 walioandikishwa mwaka 2012.

No comments:

Zilizosomwa zaidi