Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis
Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
asihudhurie kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, ila
ikiwa itaahirishwa.
Katika azimio lao viongozi wa Afrika walisema
kuwa kiongozi yeyote wa taifa asishitakiwe kuhudhuria mahakama yoyote ya
kimataifa wakati yuko madarakani.
Kesi ya Rais Kenyatta ambaye
anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu inatarajiwa kuanza
mwezi ujao mjini Hague, ingawa ameomba mara kadha kwamba iahirishwe.
Bwana Kenyatta siku zote amekuwa akisema kwamba atashirikiana kikamilifu na ICC.
AU inaishutumu ICC kuwa na kigeugeu - kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.
Hapo awali Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Dessalegn, alisema kesi za ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Omar
al-Bashir wa Sudan zinaweza kuzuwia juhudi za kuleta amani na mapatano
katika nchi zao.
Mkutano huo umemalizika.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment