Thursday, September 12, 2013

PICHA MBALIMBALI ZA MCHEZAJI OZIL AKIFANYA MAZOEZI NA TIMU YAKE MPYA YA ARSENAL


article-2418525-1BC6CCA6000005DC-387_634x343
Kiungo mchezeshaji mpya wa Arsenal Mesut Ozil hii leo alianza rasmi mazoezi akiwa na klabu yake mpya baada ya usajili wake wa paundi milioni 42.5 toka Real Madrid .
Ozil ambaye majuzi aliiongoza Ujerumani kuifungia San Marnio 3-0 huku yeye mwenyewe akifunga bao moja alionekana mwenye furaha akiwa na wachezaji wenzie ambao ndio kwanza alikuwa anajenga mazoea nao.
1184974_571115146289630_493318722_n
Ozil alipokuwa anatambulishwa mbele ya waandishi wa habari mchana huu.
Ozil alipokuwa anatambulishwa mbele ya waandishi wa habari mchana huu.
Ozil aliingia mazoezini akiwa ameambatana na Mjerumani mwenzie Per Mertesecker pamoja na kocha Arsene Wenger na msaidizi wake Steve Bould kabla ya kuanza mazoezi hayo ambapo muda mrefu alionekana akiwa karibu na Metersecker ambaye kwa vyovyote atakuwa akimsaidia kuzoea mazingira ya London .
article-2418525-1BC6CCAD000005DC-609_634x435
Wawili hao (Ozil na Metesecker) ni wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani na majuzi walikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa mabao matatu bila uliowafanya Ujerumani kukaribia kukata tiketi ya michuano ya kombe la dunia ambapo wote wawili walifunga .
Mesut Ozil anatarajiwa kuanza mchezo wa Arsenal dhidi ya Sunderland utakaopigwa huko Stadium Of Light siku ya jumamosi.
Katika hatua nyingine baba mzazi wa Mesut Ozil Mustafa Ozil ametishia kuiburuza klabu ya Real Madrid mahakamani kwa kitendo cha kuchafua jina la mwanaye .
article-2418525-1BC6BFCB000005DC-742_306x423
article-2418525-1BC6BF47000005DC-3_306x423
article-2418525-1BC6BF60000005DC-935_306x423
article-2418525-1BC6BF60000005DC-935_306x423
article-2418525-1BC6BFC0000005DC-433_306x423
article-2418525-1BC6CBA9000005DC-800_634x558
article-2418525-1BC6BE10000005DC-999_634x451
1236804_571097289624749_2088639001_n
Baba huyo amesema kuwa amekerwa na kitendo cha Real kutoa kauli ya kwamba Ozil aliuzwa kutokana na tabia ya kupenda wanawake na starehe kuliko kujituma uwanjani.
Mustafa Ozil alihoji kuwa kama mwanaye alikuwa mpenda satrehe na Real ilimuuza kwa sababu ya kupenda wanawake kwanini alikuwa akipangwa na makocha wa timu hiyo kwenye mechi .
Hivi karibuni jarida la El Mundo lilichapisha makala iliyokuwa inahusu mienendo ya Oizl ambaye inasemekana alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Mrembo toka Venezuela taarifa ambayo iliungwa mkono na Rais wa Real Florentino Perez.

No comments: