Haaaa
haaaa...ukitaka kubana pua kabane nyumbani kwenu,hapa ni hip hop
tuuu.....Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego wakioneshana umahiri umwamba
wa jukwaani na msanii mwenzake Dimond kupitia wimbo wa Muziki Gani.
Mmoja
wa wasanii wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva a.k.a
hip hop,Stamina akiwaimbisha wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake
waliojitokeza kwa wingi usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri,wakati
tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.
Msanii
mahiri ambaye kwa sasa anasumbua vilivyo anga ya muziki wa
Bongofleva,Diamond akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha
la serengeti fiesta 2013,linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa
Jamuhuri.
Sehemu ya mashabiki wakishangweka vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Mmoja
wa wakongwe wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wateule
Skwadi,atambulikae kwa jia la kisanii Mchizi Mox akiimba jukwaani usiku
huu.
Maelfu ya Watu wakiwa kwenye uwanja wa jamuhuri,usiku huu wakishangweka na tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Mkali mwingine wa Bongofleva,Dullysykes akiimba jukwaani usiku huu wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea.
Young
Killer na Stamina kama kawaida yao wakilishambulia jukwaa la fiesta
usiku huu,huku maelfu ya watu wakiwa ndani ya uwanja wa Jamuhuri,mkoani
Ni burudani murua kabisa usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.
Mwanadada
ambaye wengi wanadai amerithi viuno na sauti kutoka mwanamuziki Ray
C,anaitwa Rachael kutoka nyumba ya vipaji a.k.a THT akiimba jukwaani
huku akionesha umahiri wake wa kukata mauno.
Mkongwe
wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Afande Sele a.k.a Baba Tunda
a.k.a Simba Mzee akidhihirisha ukongwe juu ya steji ya tamasha la
Serengeti linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani
Dodoma,ambapo maelfu ya watu washabiki wamejitokeza kushuhudia tamasha
hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Makamuzi yakiendelea usiku huu
No comments:
Post a Comment