Sunday, September 1, 2013

MOTO UMERIPUKA NA KUUNGUZA JENGO JIJIN DAR..

Moto umeripotiwa alfajiri ya kuamkia Jumapili ya leo katika jengo moja lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwenye mtaa wa Samora na Mkwepu Street.

Kikosi cha Polisi kilifika mapema baada ya kupokea taarifa hizo na kisha kikosi cha zimamoto kilifika kikiwa na huduma moja tu ya gari la maji ya kusaidia kuzima moto huo.

Juhudi hizo ambazo kwa hakika hazikukidhi haja, zililazimu kuomba usaidizi wa kikosi cha zimamoto cha kampuni binafsi ya Knight Support.

Hadi taarifa hii inachapishwa (alfajiri ya saa kumi) juhudi za kuuzima kabisa moto huo zilikuwa bado zikiendelea.

Nimapema sana kufahamu chanzo na hasara iliyosababishwa na moto huo.

No comments:

Zilizosomwa zaidi