Sunday, September 8, 2013

JB ATOA SABABU ZA KUWEPO KWA FILAM MBOVU TANZANIA..

Mwigizaji mahiri nchini, Jakob Steven ‘JB’ amesema kuwa haamini katika wasanii wanaofanya kazi zaidi ya moja katika kuandaa filamu.
Alisema mshika mawili siku zote moja humponyoka na hiki ndicho kinachotokea kwenye filamu nyingi hivi sasa.
“Kumekuwa na kazi nyingi ambazo hazina ubora hii inatokana na zilizo nyingi kufanywa na mtu mmoja au wawili,ambapo kuigiza yeye,mwongozaji yeye,mpigapicha yeye, sauti mwenyewe, na vitu kama hivyo ambavyo huchangia sana kuzitia doa kazi nyingi,”alisema JB.
Aidha, alifafanua kuwa licha ya kupunguza gharama kwa kuchukua kikosi kazi kidogo, lakini kuna baadhi ya mambo ni lazima yawe na wataalamu na siyo kufanywa kienyeji.
Aliongeza kuwa wasanii wenyewe ndio wana sababu ya kukemea vitu hivi kwa kuwa wakifanya vitu vizuri, wanawafanya mashabiki kuzipenda kazi za msanii husika na kazi za nyumbani kwa ujumla.
Aliongeza kuwa siyo kwamba kazi zao ni mbaya sana, lakini zinakosa ubora kutokana na kuwa na akili ya kichwa kimoja,haiwezi kulingana na kazi ambayo inafanywa na akili za zaidi ya mtu mmoja.

No comments:

Zilizosomwa zaidi