Shirikisho
la kimataifa la soka FIFA limetoa viwango vya ubora wa timu za taifa
vya kila mwezi huku vikiwa na mabadiliko kadhaa yanayoashiria kupanda na
kushuka kwa viango kwa baadhi ya timu .
Viwango
hivyo vinaonyesha kuwa timu ya taifa ya Hispania imeendelea kuongoza
ikiwa kwenye nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina ambao wamepanda
kwa nafasi mbili toka nafasi ya nne kwa mwezi uliopita .
Hispania
wameshikilia nafasi ya kwanza kwa karibu miaka mitatu wakiwa na rekodi
ya matokeo mazuri kwenye asilimia kubwa ya michezo yake rasmi ya
kiushindani na ile ya kirafiki.
Nafasi ya tatu na ya nne zimekwenda kwa Ujerumani na Italia huku Colombia ikikamilisha orodha timu tano bora duniani .
Ubelgiji
ambao kwa sasa wanajivunia kuwa na kundi la wachezaji wenye vipaji vya
hali ya juu wanaounda timu yake ya taifa imepanda kwa nafasi nne toka
nafasi ya kumi kwa mwezi uliopita wakiwa mbele ya Uruguay na Brazil
zinazoshika nafasi za saba na nane .Brazil wamepanda toka nafasi ya tisa
huku Uruguay wakiwa wamepanda kwa nafasi tano toka nafasi ya 11 .
Orodha
ya timu kumi bora inakamilishwa na timu za Uholanzi na Croatia
zinazoshika nafasi ya tisa na nafasi ya kumi . Uholanzi wameshuka kwa
nafasi nne toka nafasi ya tano mwezi uliopita na Croatia wameshuka kwa
nafasi mbili .
Timu
ya taifa ya England imeendelea kushuka kadri siku zinavyozidi
kuongezeka wakiwa kwenye nafasi ya 17 toka nafasi ya 13 . England
waliwahi kufikia mpaka nafasi ya tatu mapema mwaka huu lakini kutokana
na matokeo mabovu ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata imeendelea kushuka
kwenye viwango vya ubora .
Kwa
bara la Afrika viwango hivyo vinaonyesha kuwa timu ya taifa ya Ivory
Coast inashika nafasi ya 19 ikiwa imeshuka toka nafasi ya kumi na nane
ikifuatiwa na Ghana ambayo imeshika nafasi ya 24 kama ilivyokuwa mwezi
uliopita .
Algeria
, Nigeria na Mali zinakamilisha orodha ya tano bora huku Cape Verde
wakizidi kupanda wakiwa kwenye nafasi ya sita . Misri , Burkina Faso , Cameroon,Senegal na
Afrika kusini bzinamalizia top 10 ya bara la Afrika huku Tanzania ikiwa
kwenye nafasi ya 37 kwa Afrika na 127 kwa Dunia ambapo imepanda kwa
nafasi moja .
No comments:
Post a Comment