Tuesday, September 24, 2013

BOMU LARUSHWA, LALIPUKA ZANZIBAR


Watu wasiojulikana juzi walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na kulipuka kwa kutoa moshi mkali katika maeneo ya Darajani mjini hapa.
Tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na  inadaiwa wakusika kuwa walikuwa katika gari aina ya Pick up.
Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema bomu hilo lilikuwa muundo wa soseji ambalo lilirushwa katika duka la Sahara Store lililopo Darajani na kuangukia katika kreti zenye chupa ya soda.
Alisema mmoja wa walinzi aliyekuwapo eneo hilo, Amour Kassim, aliuchukuwa mlipuko huo huo ambapo ndipo ulipoanza kutoa moshi mwingi na kuurusha barabarani na kwamba ulisababisha kishindo, kikubwa na barabara kuchimbika.
Alisema kitu ambacho kitaweza kusaidia uchunguzi wa Jeshi la Polisi ni masalio ya unga mweupe na kokoto zilizochimbika na kuwataka wananchi kuwa watulivu kwani vyombo vya ulinzi na usalama tayari vimeshaimarisha ulinzi.
Alisema katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa wala wahalifu wa tukio hilo kukamatwa, hivyo aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazoweza kusaidia kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo ambalo linachochea kuleta hofu na taharuki kwa wananchi.
Chanzo: Nipashe

No comments: