Tuesday, September 24, 2013

BALOTELI AKOSA PENATI KWA MARA YA KWANZA KATIKA MAISHA YAKE, SASA ATUPWA JELA

Mario Balotelli alizuia na wachezaji wenzake asimfuate mwamuzi mara baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Napoli
KLABU ya AC Milan itasafiri kwenda kuivaa timu ya Juventus mapema mwezi ujao bila ya mshambuliaji wake, Mario Balotelli baada ya kufungiwa mechi tatu kutokana na kufanya vurugu baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Napoli uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshambuliaji huyo alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo huo ambao walilala kwa mabao 2-1, Balotelli hakukubaliana na kadi hiyo na kuanza kumzonga mwamuzi.
Chama cha soka nchini Italia imemfungia michezo mitatu kutokana na kitendo chake cha kushambulia mwamuzi hivyo ataikosa michezo mitatu ikiwemo ule wa Juventus pamoja na Bologna na Sampdoria.
"Adhabu hiyo imetolewa kwa Balotelii kutokana na vitendo vyake vya kukwaruzana na wachezaji wa timu pinzani, mwamuzi wa akiba pamoja na kutokukubaliana na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo,” alisema mmoja wa maafisa wa chama hicho akifafanua adhabu  hiyo.


 Faulo iliyosababisha Balotelli kupewa kadi ya pili ya njano na kisha nyekundu

No comments: