Mahakama nchini India imewahukumu wanaume wote wanne
kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumuua mwanamke katika
basi katika mji mkuu wa India Delhi mwezi Desemba mwaka jana.
Mmoja wao aliangua kilio na kuanguka baada ya kutangazwa kwa hukumu dhidi yao .
Msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 aliumizwa sana na baada ya wiki moja alifariki kutokana na majeraha .
Karibu miezi 9 baada ya ubakaji ulioitikisa
India, jaji ametoa hukumu kwa wanaume wote wanne ambao tayari walikuwa
wamepatikana na hatia ya uhalifu .
Wendesha mashtaka walikuwa wamewaombea hukumu ya
kifo wakisema ingetoa ishara muhimu kwamba uhalifu wa aina hiyo
hautakubalika kamwe .
Familia ya mwanamke huyo pia waliomba wanaume hao wanyongwe .
Lakini mawakili watetezi wa wanaume hao
walipinga mapendekezo ya hukumu ya kifo , wakisema wateja wao hawakuwa
na rekodi za uhalifu awali na kwamba wanastahili kusamehewa .
Kifo cha mwanafunzi huyo mwezi Disemba mwaka
jana kilisababisha maandamano makubwa ya upinzani kote nchini India ,
yaliyoilazimisha serikali kubadili sheria zilizokuwepo za uhalifu wa
ngono
BBC
No comments:
Post a Comment