Wednesday, September 11, 2013

AFISA ELIMU KATAVI AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KUANGALIA MITIHANI DARASA LA SABA

WANAFUNZI NJE YA DRS 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Muungano na Mpanda katika wilaya yam panda wakiwa nje ya Madarasa muda mfupi mara baada ya kumaliza mtihani wa somo la sayansi lililoanza asubuhi   kama walivyokutwa na mpiga 

 WATAALAM NA WANANCHI 
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Tukoma wakiwa na Afisa Elimu Mkoa wa Katavi wakijadili mstakabali wa ujenzi wa madarasa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa na Nyumba za walimu shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za mwalimu na vyumba madarasa hali inayofanya darasa moja kusomea wanafunzi 246 wa shule hiyo ya Tukoma wakisoma kwa zamu, shule inawatoto kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na mwaka huu watoto saba yu ndio waliofanikiwa kufanya mtihani wa darasa la saba.
MTIHANI TUKOMA WATOTOWanafunzi wa darasa la Saba wakiwa Darasani wakifanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi wanafunzi hao ni wa shule ya msingi Tukoma Wilaya ya Mlele .
(Picha zote na Kibada Kibada)
………………….
Kibada Kibada-Mpanda KATAVI
Afisa Elimu wa Mkoa wa Katavi Ernest Hinju amefanya ziara ya kushitukiza kwa baadhi ya shule za msingi katika wilaya ya Mpanda na Mlele na kuridhishwa na hali ya mtihani inavyoendelea baada ya kukuta   hali ya mtihani inaendelea vizuri na hakuna matatizo yeyote.
Afisa Elimu huyo alianza kwa kutembelea shule ya Msingi Tukoma ambayo imekuwa na changamoto nyingi  ikiwemo kuwa na chumba kimoja cha madarasa hivyo kufanya wanafunzi kuka chumba kimoja wakati wa kujifunza na kuleta changamot nyingi na kugonga vyomba vya habari  hivyo kufanya uongozi kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi.
  Katika ziara yake hiyo fupi alifuatana na Mkaguzi wa shule za Msingi  na Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa na Afisa Habari   ili kujionea hali inavyoendelea katika maeneo mbalimbali ya shule za msingi ambazo wanafunzi wanaendelea kufanya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba kumaliza elimu ya Msingi.
Kwa upande wa Mkoa wa Katavi hali inaendelea vizuri na hakuna taarifa zozote zimeripotiwa za kutokea kwa matukio mabaya hali inaendelea vizuri.
 Afisa elimu Mkoa wa Katavi Ernest Hinju akiwaongea na mwandishi wa Habari hizi muda mfupi baada ya kutembelea shule mbalimbali za msingi zinazoendelea kufanya mtihani na kukuta hali iko shwari bila matatizo yeyote.
Baadhi ya shule zilizotembelewa kwa mkoa wa Katavi ni Shule ya Msingi Itenka B’Shule ya Msingi Dirifu na SHULE YA Msingi Tukoma ambazo zote ziko katika wilaya ya Mlele.
Shule nyingine zilizotembelewa ni shule ya Msingi Kashato,Katavi,Azimio,Mpanda Muungano,Majengo na shule ya Msingi Nsimbo ambazo ziko katika Wilaya ya Mpanda na zote hali ilikuwa shwari.

No comments:

Zilizosomwa zaidi