Thursday, August 29, 2013

WATUMISHI WA VIJIJI NA KATA WILAYANI MULEBA WAULAMBA KWA KUWAPEWA VYOMBO VYA USAFIRI





 Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imewapatia vyombo vya usafiri watumishi wake ngazi ya kata na vijiji ili waweze kutekeleza majukumu na malengo ya halmashauri hiyo kuleta maendeleo ya wananchi kwa haraka.

Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya hiyo Oliva Vavunge amesema hayo Agosti 01,kuwa watendaji wa kata 18 wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya Tsh. 39 mil na wahudumu wa Afya vijijini 45 wamepatiwa Baiskeli zilizogharimu Tsh.8.1 mil

Vavunge amesema kuwa fedha zilizotumika kununua vyombo hivyo vya usafiri ni kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na watumishi hao wamekopeshwa na watakuwa wakikatwa fedha kutoka katika mishahara yao ili kwa awamu nyingine watendaji wa kata 13 waweze kukopeshwa

Aidha amesema halmashauri kupitia idara ya kilimo imenunua trekta kwa kiasi Tsh.milioni 42 ambapo kwa atakayelihitaji kulitumia kwa kilimo na atalikodi kwa ekari moja Tsh.60,000/=.

Naye Afisa mtendaji wa kata ya Biirabo Boaz Musasa ameshukuru kwa niaba ya wenzake kupatiwa pikipiki na kwamba katika kata yake amehudumia vijiji vyenye maeneo mapana yaliyo na mabonde na milima.

Akikabidhi vyombo hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw George katomelo amewahimiza kuhakikisha watumishi hao wanavitumia kwa malengo yaliyokusudiwa licha ya kuwa mali yao baada ya makato katika mishahara yao.

No comments:

Zilizosomwa zaidi