Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamebainisha kuwa wanawake
wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya
kuvamiwa usiku wa kuamkia leo.
Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume
wawili waliwatendea kitendo hicho wanawake hao Katie Gee na Kirstie Trup, wote wenye
umri wa miaka 18 kutoka London, walipokuwa wakitembea
katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
Wanawake hao ni walimu wa kujitolea wakifanya kazi kisiwani humo
Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi ya wanaume hao.
Katika taarifa yake shirika la usafiri la i-to-i nchini Uingereza lilisema kuwa wanawake hao wameondoka hospitalini.
Polisi wanasema kuwa wanawake hao wenye umri wa
miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar ambao
ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili
waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagiwa Acid kwenye mikono , vifua
na nyuso zao.
Wanawake hao walipelekwa kwa ndege hadi Dar es
Salaam ambako walipokea matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema kuwa
majeraha yao sio makubwa sana ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao.
Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka wahusika.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment