Abiria
wakiwa tayali wameshuka katika Daladala baada ya kutoka maeneo
mbalimbali ya mji wa Dodoma na kushushiwa Barabarani baada ya kukuta
msongamano mkubwa katika stand mpya iliyoanza kutumika leo ya jamatini.
Mmoja wa viongozi wa
wafanyabiashara Ndogondogo Danny Msitewa akifafanua jambo alipokuwa
akisoma majina na kuwapa namba za utamburisho wa nafasi za kuweka
vibanda vyao katika stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma
Wafanya biashara waliokuwa stend
iliyokuwa ya muda ya daladala oil com wakikusanya bidhaa zao
zilizosambazwa na tingatinga lililofika kubomoa vibanda walivyokuwa
wakaifaanyia biashara zao ili kuwashinikiza kuondoka eneo hilo.
Asikari akitoa maelekezo kwa
baadhi ya watu waliokuwa wakivizia kukwapua mali za watu zilizozagaa
stand ya Daladala ya oil com Baada ya kubomolewa vibanda vyao ili wahame
katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Mipango miji na
Mazingira manispaa ya Dodoma Stephen Mwanga akiwatangazia wafanya
biashara ndogondpgo kutoendelea na ujenzi mpaka baazi ya taratibu
zitakapokamilishwa.
Msukuma Tololi akiingiza moja ya
vibanda vya wafanyabiashara katika Stand mpya ya Daladala ya Jamatini
Dodoma iliyoanza kutumika leo
Magali ya Daladala yakisubili
abiria ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo
huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria
barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
Daladala
zikisubili kuingia ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza
kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha
kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
MWENYEKITI wa kamati ya Mipango
miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi
wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya
Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa
kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya
kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya
watumiaji wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji wa Dodoma.
Mwenyekiti huyo amewataka
kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana
na kile alichosema ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu
kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.
Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo
hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia
kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi wao
walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo
haujaanza Augost 2012.
Baada ya kufika na kujionea
kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali
halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda
lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa
ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.
'' Nimesimamisha ujezi usiendelee
kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu
ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa
manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga
kwa upande wao baadhi ya Machinga
hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia
majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa hata
wakati stend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi hizo
zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.
No comments:
Post a Comment