Roberto Soldado |
Mshambuliaji mpya wa Tottenham Spurs Roberto Soldado ameanza
vema kibarua chake katika timu hiyo kwa kuonyesha umahili wake wa kutikisa
nyavu akiwa ameeshafunga mabao manne katika michezo mitatu aliyoichezea Tottenham.
Soldado amefunga goli lake la nne leo likiwa
ni goli pekee lililoipa ushindi Tottenham dhidi ya Swansea.
Wiki iliyopita wakati wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu
nchini Uingereza dhidi ya Crystal Palace, Soldado alifunga goli pekee kwa
mkwaju wa penalty ambalo pia liliipa ushindi timu yake.
Soldado amesajiliwa akitokea Valencia
kwa uhamisho wa ada ya 30 million euros ($40 million).
Magoli ya Soldado yanatoa hofu kwa Tottenham juu ya kumkosa
mshambuliaji wake Gareth Bale anayehofiwa kutaka kutimkia Real Madrid.
By: Mligo G
No comments:
Post a Comment