Mwaka huu shindano la kusaka vipaji
vya kuimba maarufu kama Epiq Bongo Star Search litakuwa likioneshwa kupitia TBC1.
Kupitia Facebook, Rita Paulsen (Madam Rita) ambaye ni mwanzilishi na jaji mkuu wa shindano hilo ametoa
sababu mbili za kuhamisha matangazo hayo kutoka ITV hadi TBC1.
“Baada ya kusoma maoni yenu,
ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013
kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1.
Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara
ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya
pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye
ving’amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku''.
No comments:
Post a Comment