Tuesday, August 20, 2013

MIKOA YA SHINYANGA NA MARA YAONGOZA KWA NDOA ZA UTOTONI...

Imebainika kuwa mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa ndoa za utotoni kwa asilimia 59 ukifuatiwa na mkoa wa Mara ambao ndoa za utotoni ni asilimia 55 kwa Tanzania.

Chanzo cha ndoa hizo za utotoni ni kutokana na wazazi wengi katika mikoa ya Shinyanga na Mara huwaposa watoto wao mapema iwezekanavyo ili waweze kujipatia ng'ombe pesa kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kilimo na ufugaji.

Kukithiri kwa ndoa hizi za utotoni kumesababisha kupungua kwa idadi ya watoto wanaokwenda shule kwa kipindi cha hivi karibuni kwani wazazi wengi wanaamini kuwa wanapoteza pesa na mda kwa watoto wao wa kike kwakuwapeleka shule.

No comments:

Zilizosomwa zaidi