Kundi la waasi wa M23 katika Jamhuri
ya kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa linasimamisha mapigano mara moja,
kuruhusu uchunguzi juu ya makombora yaliyovuka mpaka na kuanguka katika
nchi jirani ya Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert Mende, ameiambia DW mjini Kinshasa kuwa serikali ya nchi hiyo haijashangazwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.(P.T)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert Mende, ameiambia DW mjini Kinshasa kuwa serikali ya nchi hiyo haijashangazwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.(P.T)
Jana, Rwanda ililishutumu jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kile ilichokiita uchokozi wa
makusudi, baada ya kombora linaloaminika kutoka upande wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kuanguka nchini Rwanda, na kumuuwa mwanamke mmoja
na kumjeruhi vibaya mtoto wake mchanga.
Serikali ya Kongo ilizikanusha mara
moja tuhuma hizo, ikisema zilikuwa zikiashiria azma ya Rwanda kujiingiza
waziwazi katika vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
Kikomo cha uvumilivu
Kufuatia kifo cha mwanamke huyo katika
mji wa Rubavu kaskazini magharibi mwa Rwanda, wizara ya mambo ya nje ya
Rwanda ilitoa tangazo ambalo limesema nchi hiyo inao uwezo wa kujua
yalikotoka mashambulizi dhidi yake, na kuonya kuwa haitasita kulinda
eneo lake na kuwatetea wananchi wake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda,
Louise Mushikiwabo, amesema katika kipindi cha mwezi mmoja, jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limerusha mabomu yapatayo 34 ndani ya
Rwanda. ''Tumejizuia tuwezavyo kuchukuwa hatua, lakini sasa hatuwezi
kuendelea kuvumilia uchokozi huu.'' Amesema Bi Mushikiwabo.
Kongo yasema ni kisingizio
Akijibu tuhuma kutoka Rwanda kuwa
jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndilo linalorusha mabomu
yanayoanguka nchini Rwanda, Waziri Mende amesema tuhuma hizo zinalenga
kuhalalisha kujiingiza tena katika mikoa ya Kivu. ''Inachoazimia Rwanda
ni kusababisha vurugu isiyokwisha ili iweze kuendelea kupora mali katika
mikoa ya kivu, kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa miaka 15 iliyopita,''
alisema Mende.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa
ulisema jana kwamba unazo ''ripoti za kuaminika'' za kuaminika, ambazo
zinaonyesha kuwa wanajeshi wa Rwanda wameingia katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Rwanda kuwasaidia waasi wa M23, katika vita linayopigana
dhidi ya jeshi la Kongo na wanajeshi wa kulinda amani nchini humo,
MONUSCO.
Aidha, afisa wa ngazi ya juu wa
MONUSCO, Ray Vilgilio Torres amesema vikosi vyao vimepata uhakika kuwa
bomu lililomuuwa mwanamke nchini Rwanda, lilirushwa na waasi wa M23,
kutoka ngome yao ya msitari wa mbele ya Kibati.
No comments:
Post a Comment