Bandari
ya Mwanza Kaskazini na Kusini yachafuka ni kutokana na mgomo wa
wafanyabiashara na watu wanaofanya shughuli za kubeba mizigo
(Makuli) kugomea kutozwa VAT mala mbili ya kupakia na kupakua mizigo
yao, ushuru na makato mengine na kusababisha shehena ya mizigo kutoka
Bukoba kukaa ndani ya meli kwa masaa 7 Bandarini hapo Jijini Mwanza.
Sakata
hilo lilitokea jana kuanzia majira ya saa12:30 na kudumu hadi saa 7:00
mchana baada ya Meli ya Mv Victoria kuweka Nanga kwenye Bandari ya
Mwanza Kaskazini kufatia Mamlaka ya Bandari nchini( TPA) kutoa maelekezo
kwa uongozi wa TPA Mwanza kuwa muda wa mzabuni aliyekuwa akifanya kazi
za kupakia, kupakua na kutoza ushuru wa mizigo kumaliza muda wake na
kazi hiyo kufanywa na Mamlaka hiyo.
Akizungumza
wakati wa kutekeleza mgomo huo Mwenyekiti wa Ushirika wa Wahudumu wa
Bandari ya Mwanza Kaskazini na Kusini Rajabu Said alisema kuwa wao
waliokuwa wazabuni wa kufanya shughuli za kupakia, kupakua na kutoza
ushuru wa mizigo Bandarini hapo kugomea na TPA kuendelea na kazi hizo
kutokana na muda wa miaka miwili waliokuwa wamepewa kumalizika na
kutakiwa kutjishughulisha tena.
Mwenyekiti
Said alieleza kuwa kutokana na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kutoa
mwongozo wa ukusanyaji mapato na ushuru baada ya kumalizika kwa muda wa
USHIRIKA wa miaka miwili uliokuwa umetolewa kwa zabuni ambayo walishinda
mwaka 2011 hadi kumalizika Agosti 30 mwaka huu aligubikwa na mizengwe
na kuwa na usiri na kutowekwa bayana na viongozi wa TPA Mwanza.
Baada
ya Kikao hicho kumalizika kwa makubaliano yaliyoafikiwa jambo la
kushangaza asubuhi ya leo Agosti 31 mwaka huu wakati tulipofika
Bandarini Mwanza Kaskazini tulikuta utaratibu mpya kwa walinzi wa
Kampuni ya Ulinzi ya SUPREM na kuteleleza kuwa haturuhusiwi kufanya
shughuli za kutoza ushuru, kutoza mizigo tutakayo pakua leo Jumamosi
(Jana) na kupakia Jumapili na kazi hiyo iko chini ya TPA kuanzia sasa.
Said
alisema baada ya taarifa hiyo tulipinga na kuwataka wafanyabiashara wa
kutoka Mjini Bukoba kuacha kushusha mizigo hiyo hadi muafaka upatikane
na wao waliafiki kwa kutuunga mkono kutokubaliana na uongozi wa TPA kwa
vile ulilenga kuwatoza fedha zaidi kwa kulipia VAT mala tano kwa mizigo
yao ikiwa ni kupakia kulipa VAT asilimia 18 kwa Marine na TPA ikiwa na
kushusha na tozo la fedha za Makuli hao.
“Hatukubaliani
na kabisa na kilichofanywa na uongozi wa TPA kwani zabuni haijatangazwa
nasi tukapata kutuma maombi yetu lakini imedaiwa kuwa kuna Chama cha
Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (TPA) Mwanza (DOWUTA) wamekisajili ili
kuchukua nafasi ya Ushirika kufanya kazi hiyo na ndiyo maana Tenda
hawajaitangaza na tumeelezwa na uongozi kuna mzabuni tayari nasi
tumepinga na kugomea kukubaliana na utaratibu huo hivyo Bandari zote
Makuli tumeomba uwazi uwepo na tenda zitangazwe” alisisitiza.
Ushirika
huo wenye jumla ya wanachama 3000 na ulisajiliwa na kufanya kazi hizo
Bandari za Mwanza Kaskazini na Kusini baada ya kushinda zabuni hiyo
mwaka 2011 ulipunguza tatizo la ajira na kuwafanya wanachama hao ambao
ni wafanyakazi wa kubeba mizigo wamekuwa na utaratibu wa kukopeshana,
kuchaniana kwa matatizo ya ugonjwa na kutoa fedha kwa mwanachama
anayefariki na wanaositaafu kubeba mizigo hulipwa milioni 1.5 ikiwa na
hisa yake ya uanachama hivyo kutopewa kazi hiyo imedaiwa kuongeza watu
kujihusisha na uhalifu mitaani na kuweka mashaka kwa wasafiri na mizigo
yao kuanza kuibiwa na watu kwa kukabwa nakati za usiku na asubuhi.
Baada ya vuta ni kuvute kutoka kwa wafanyabiashara na uongozi wa
TPA Mwanza na Makao Makuu iliyotuma wawakilishi wake kujadiliana na kuona jinsi
ya kumaliza mvutano huo na kumaliza mgomo wa Makuli hao na kupelekea kuibuka
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Huduma wa TPA Clementi Kiloyavaha na kueleza kuwa
utaratibu uendelee kwa leo kama ilivyokuwa wakati wakianda Kikao cha pamoja.
Kiloyavaha alisema kwamba kutokana na maelekezo kutoka kwa Waziri
wa Uchukuzi Dr.Harison Mwakyembe kwa Mamlaka hiyo ya TPA wamepewa utaratibu na
hivyo utaanza kutekelezwa kuanzia Septemba mosi na kunachotakiwa kufanyika ni
kikao cha pamoja baina ya wadau wa TPA na Wafayabiashara wanaotumia Bandari za
Mwanza Kaskazini na Kusini kuwapa utaratibu mpya.
Kwa upande wa wafanyabiashara baadhi yao waliozungumizia sakata
hilo na kukataa kutajwa majina yao walisema kuwa wao wanapinga kutozwa VAT
asilimia 18 kwa kila tani moja na vifurushi wakati wa kupakia na kupakua mala
mbili ikiwa ni kwa Kampuni ya Meli ya Marine na Mamlaka ya Babdari TPA pamoja
na kutozwa VAT ya fedha za vibarua wa kupakia na kupakuwa wanayolipia kuwa ni
kero kubwa kwao.
“Hili litatufanya kuacha kupitisha mizigo yetu katika Bandari hizi
za TPA kwa vile utaratibu huu umelenga kuturudisha nyuma na kutukamua zaidi na
kukosa faida kabisa na leo tumepoteza wateja na tutauza ndizi,mihogo na matunda
kwa bei ya hasara na hili limetukera sana nibora wangetuarifu kwa matangazo
badala ya kukurupuka na kuamua hata kama ni maagizo ya Waziri Mwakyembe” walisema
.
Hali ililejea majira ya saa 7:00 mchana makuli na wafanyabiashara
kuendelea na utoaji wa bidhaa zao na kupakia baada ya kuishusha ili iliyotoka
Mji wa Bukoba na kusababisha mgomo wa masaa 7 na kuasilika kwa makundi ya
wafanyabiashara wa ndizi mbivu na mbichi, matunda na mihogo katika masoka
mbalimbali ya Jiji la Mwanza kama ilivyozoeleka Meli ya Mv Victoria inapofika
Jijini Mwanza toka Mjini Bukoba.
No comments:
Post a Comment