![]() |
Ndg Joseph Warioba |
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph
Warioba, ametaka wenye ndoto ya kuwa na Katiba ya Tanganyika, kusubiri
hadi muundo wa Serikali tatu utakapokubalika.
Jaji Warioba, alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma
wakati akifungua baraza la wawakilishi la watu wenye ulemavu ambao
wanaendelea kutoa maoni yao mjini hapa.
Alisema kuwa tume inayo mawazo ya Tanzania na
ukiacha suala la Muungano, Zanzibar wamejikita zaidi kwenye muungano
mengine yote yaliyo humu na migogoro mingine yanatoka Tanzania Bara.
“Wakitaka kutunga Katiba yao sijui kama watakuwa
na maoni tofauti kuhusu haya, utakuta ni haya haya, kama wataongeza
madiwani lakini hata hayo tayari yapo katika kumbukumbuku,” alisema
Warioba.
Mjumbe huyo alisema iwapo wananchi wataamua kuwa
na muundo wa serikali tatu wanaweza kutumia mawazo yaliyokusanywa wakati
wa mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Alisema tume yake inahifadhi
kumbukumbu rasmi za maoni ya wananchi wote ambapo sura na sauti za
Watanzania waliotoa maoni zimehifadhiwa ili kujua wanachokitaka.
Kuhusu mfumo wa kukusanya maoni katika mabaraza ya
Katiba ulioandaliwa na tume, alisema ni kuwagawa wananchi katika
makundi kisha hugawiwa sehemu za rasimu kwa ajili ya kupitia kila
kipengele, alikiri changamoto ambazo wanakabiliana nazo ni kuingiliwa
kwa mchakato huo.
No comments:
Post a Comment