Jeshi
la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni majambazi
tisa wa kutumia silaha akiwemo askari polisi wa kituo cha polisi
Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Bw. Suleimani Kova amesema
majambazi hao wamekamatwa katika operesheni maalum ya jeshi hilo ambapo
pia walifanikiwa kukamata sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ)
zinazoaminika kutumika katika uhalifu pamoja na silaha na risasi.
Pia Kamanda kova ameeleza kukamata magari yanayosadikika kutumika katika
uhalifu tofauti pamoja na yenye namba za usajili T865 CEH aina ya Carina,
na T967 AUG Carina.
CHANZO: ITV
No comments:
Post a Comment