UGONJWA USIOFAHAMIKA JINA, UMEIBUKA NA KUSHAMBULIA
ZAO LA MIGOMBA KATIKA KIJIJI CHA SHUNGA KILICHOPO KATA YA BUHORO WILAYANI
KASULU MKOANI KIGOMA
HAYO YAMEBAINISHWA NA TIMU YA BLOG HII ILIPOTEMBELEA
KIJIJI HICHO NA KUKUTA ZAO LA MIGOMBA LIMENYAUKA NA NDIZI KUKAUKA HALI MBAYO
IMEONEKANA KUWA TOFAUTI KWA ZAO HILO
BLOG HII IKIONGEA NA BAADHI YA WAKAZI WA KIJIJI
HICHO WAMESEMA KUWA, UGONJWA HUU UMEIBUKA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA HUU AMBAPO
MIGOMBA YOTE IMESHAMBULIWA NA UGONJWA HUU HALI AMBAYO IMEPELEKEA KUKAUKA KWA
ZAO HILI
WANAKIJIJI HAO WAMEBAINISHA KUWA, HAPO AWALI UGONJWA
WENYE DALILI KAMA ZA UGONJWA HUU UNAOKAUSHA MIMEA, ULIANZA KWA KUSHAMBULIA NA
KUKAUSHA MAZAO KAMA VILE MAHARAGE NA MAGIMBI NA NDIPO MWAKA HUU UGONJWA WENYE
DALILI ZILEZILE UMEWEZA KUSHAMBUIA MIGOMBA NA NDIZI KWA UJUMLA
AKIONGEA KWA NIABA YA WANAKIJIJI WENZAKE BW. ABRAHAM
MUHUNDA AMESEMA KUWA UGONJWA HUU NI CHANGAMOTO KUBWA KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA SHUNGA NA UNARUDISHA
NYUMA MAENDELEO KWANI ZAO HILO HUTUMIWA KWA CHAKULA NA WAKATI MWINGINE KUUZWA
NA KUJIPATIA FEDHA
MPAKA SASA JINA LA UGONJWA HUU BADO HALIJAFAHAMIKA
NA JUHUDI ZA KUZUIA UGONJWA HUU BADO HAZIJAANZA
No comments:
Post a Comment