
Polisi walichukua hatua na kuwaua majambazi hao sita , kulingana na taarifa za maafisa wakuu. Polisi mmoja aliuawa.
Genge hilo la majambazi hamsini, lilitekeleza uvamizi wao mapema alhamisi.
Msemaji wa majambazi hao alisema kuwa watu
waliofanya shambulizi walikuwa wanachama wa kundi la MRC linalotaka mkoa
wa Pwani kujitenga na Kenya.Hata hivyo hakuna taarifa ikiwa watu wengine walijeruhiwa.
Kundi la MRC linasema kuwa linafanya harakati
zake kwa niaba ya watu wa eneo la pwani ambalo linasema kuwa
wamenyanyaswa na wengi wao wakiwa Waisilamu wanaosema kuwa wanahisi
kubaguliwa.
Kundi hilo liliambia BBC kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika kuwa lengo lao ni kuinua hadhi ya maisha ya watu wa Pwani
Aidha lililaumiwa kwa kufanya mashambuzlii kadhaa kabla ya uchaguzi ambapo watu 12 waliuawa.
Wiki jana msemaji wa kundi hilo alikamatwa kwa kuwa na uhusiano na kundi hilo.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment