Wednesday, March 20, 2013

RAIS OBAMA ATEMBELEA ISRAEL KWA MARA YA KWANZA.

Rais Obama Rais Barack Obama amewasili nchini Israel ikiwa ni ziara yake ya kwanza kama rais wa Marekani.

Wakati alikiwasili, waandamanaji walikusanyika na ulinzi kuimarishwa nchini Israel na katika maeneo ya Palestina.

Obama anategemewa kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa ziara yake ya siku tatu.

Mambo makuu yaliyomfanya afanye ziara hiyo ni vita nchini Syria na wasiwasi kuhusu nia za Iran za kinyuklia

No comments:

Zilizosomwa zaidi