HIZI NI BAADHI YA TIMU ZITAKAZOSHIRIKI MICHUANO YA AFCON
Afrika kusini inawania taji lake la pili
Baada ya Libya kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe,
shirikisho la soka barani Afrika liliamua mwaka jana kuwa fainali za
mwaka 2013 zifanyike nchini Afrika kusini. Timu ya nchi hiyo kama
inavyojulikana "Bafana Bafana", inaweza kutwaa taji hilo kwa mara ya
pili baada ya kuwa mabingwa mwaka 1996. Afrika kusini imo katika kundi A
pamoja na Angola, Cape Verde na Morocco.
Mabingwa watetezi Zambia
Ushindi wa kushangaza wa Zambia katika fainali za kombe la Afrika
mwaka 2012 si rahisi kuusahau haraka. Zambia iliishinda Cote d'Ivoire
kwa mabao 8-7 kwa njia ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare katika
dakika za kawaida. Zambia inacheza katika kundi C ambalo lina timu za
Nigeria, Burkina Faso na Ethiopia.
Côte d'Ivoire
Côte d'Ivoire inakwenda katika fainali hizo nchini Afrika kusini
ikiwa ni makamu bingwa. Côte d'Ivore imeishinda Senegal katika awamu ya
kufuzu katika makundi. Mjini Dakar baada ya Côte d'Ivoire kuongoza kwa
mabao 2-0, kulizuka ghasia na mchezo kuvunjika. Senegal iliondolewa.
Côte d'Ivoire inacheza katika kundi D pamoja na Tunisia, Algeria na
Togo.
Angola
Kwa mara ya saba Angola imefanikiwa kucheza katika fainali za kombe
la Afrika. Timu hiyo inayofahamika kama "Palancas Negras", ilifanikiwa
kwa kuiondoa Zimbabwe kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza na kuiadhibu
Zimbabwe tena kwa mabao 2-0 nyumbani mjini Luanda. Magoli yote mawili
yalifungwa na mshambuliaji Manucho (kulia).
Angola
Mashabiki wa Angola wameonyesha matumaini kuwa timu yao (pichani)
itafanikiwa kuvuka kikwazo cha duru ya kwanza. Wanahisi kuwa ushindi
unawezekana dhidi ya wenyeji Afrika kusini, Morocco na Cape Verde. Kocha
wa Angola, raia wa Uruguay, Gustavo Ferrín, kwa upande wake analiona
kundi A kuwa gumu zaidi.
Cape Verde
Wacape Verde wanajisikia fahari na kikosi chao cha "Nyangumi wa
Buluu", ama kama wanavyofahamika nchini humo "Tubarões Azuis". Kwa mara
ya kwanza nchi hiyo inashiriki katika mashindano makubwa ya kimataifa.
Januari 19 Cape Verde itafungua dimba la fainali hizo dhidi ya wenyeji
Afrika kusini mjini Johannesburg.
Ghana
Mara nne Ghana imekuwa mabingwa wa Afrika. Mara nane timu hiyo ya
Afrika magharibi imejikuta katika fainali. Mara ya mwisho ilikuwa nchini
Angola mwaka 2010. Ghana ilishindwa na Misri kwa bao 1-0. Mchezaji
maarufu katika timu hiyo alikuwa mchezaji wa kati André Ayew (kulia)
kutoka Olympique Marseille. Ghana imo katika kundi B pamoja na Mali,
Niger na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
No comments:
Post a Comment