WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki ametangaza
kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) waliokwamisha mradi wa kuwasaidia wafugaji wa hifadhi
hiyo ulioahidiwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2008.Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro na viongozi wa NCAA mara baada ya kuelezwa kuhusu kukwama kwa mradi huo, Balozi Kagasheki alisema lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya viongozi hao.
“Haiwezekani mradi ulioahidiwa mwaka 2008 leo hii ukwame, waliohusika kuukwamisha ni lazima wakae pembeni. Ninakwenda Dar es Salaam ila wakae wakijua kuwa barua zao zinakuja” alisema Kagasheki na kuongeza;
“Kabla sijaondolewa wizarani kutokana na matatizo kama haya, mtaondoka ninyi kwanza.…, kukwama kwa mradi huu kutawafanya wananchi wamchukie Rais Kikwete na wanasiasa,” alisema Balozi Kagasheki.
No comments:
Post a Comment