KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bunda, Dinah Rweyemamu
juzi alipatwa na wakati mgumu pale alipozomewa na wananchi
wakimshinikiza ashuke jukwaani kufuatia wananchi hao kutoridhika na
majibu aliyokuwa akiyatoa kwa maswali yao.
Dinah alifikwa na zahama hiyo muda mfupi baada ya
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Abdallah Bulembo kumwita jukwaani
ajibu maswali hayo yaliyoelekezwa kwake wakati wa mkutano wa hadhara wa
chama hicho uliofanyikia katika eneo la kituo cha zamani cha mabasi
mjini Bunda.
Swali lililomletea kizaazaa kaimu mkurugenzi huyo
ni lile lililotolewa na Alfred Ndowa aliyetaka kujua sababu za kukithiri
kwa michango kwa shule za msingi na sekondari hasa wakati wa
kuandikisha wanafuzni wa darasa la kwanza.
Bulembo alimwita Dinah jukwaani ambapo katika
kujibu alisema dhamana ya kutokuwapo au kuwapo kwa michango mashuleni
imo mikononi mwa kamati zao za shule.Kufuatia kauli hiyo ,wananchi
walianza kumzomea kaimu mkurugenzi huyo wakisema hajui kitu na kumtaka
Bulembo amshushe.
No comments:
Post a Comment