Monday, November 19, 2012

SEKRETARIETI CCM YAJA KIVINGINE

SEKRETARIETI mpya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeapa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho tawala kwa kufuatilia mienendo ya watendaji wakuu wa Serikali wakiwamo mawaziri.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mpango huo wenye lengo la kuongeza ufanisi wa Serikali, utawabana pia wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wanaosimamia utekelezaji wa Ilani hiyo.

Alisema ikibainika mtendaji yeyote wa Serikali anabaronga katika uwajibikaji wake, sekretarieti hiyo itamjulisha Rais Jakaya Kikwete na kumshauri awafukuze kazi.

“Lengo ni kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake na endapo itabainika watendaji wanaboronga, sekretarieti haitasita kumfahamisha Rais ili awatimue ama kuwaondoa katika majukumu yao,” alisema.

No comments: