Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania [MCT], Kajubi Mukajanga
alitangaza hayo na kusema timu hiyo itatoa hadharani uchunguzi huo.Bodi ya MCT,TEF iliunda tume hiyo Septemba 4, mwaka huu, iliyoongozwa na Meneja wa Utafiti na Machapisho wa MCT, John Mirenyi, wakiwemo Mhariri wa masuala ya siasa gazeti la Mwananchi, Hawra Shamte na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Simon Berege.
Mwangosi aliuawa Septemba 3 mwaka huu, kwa kupigwa na bomu na askari polisi katika kijiji cha Nyololo Mufindi mahali palipokuwa wafuasi Chadema wakati mahali hapo walikwenda kufungua tawi la chama hicho
Tayari askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Pasificus Cleophace Simon (23), mwenye namba G2573, ameshafikishwa mahakamani mkonai Iringa kwa mauaji ya mwandishio huyo.
No comments:
Post a Comment