Wednesday, October 3, 2012

Mambo ya warembo walimbwende leo hii.

  • Leo ni siku ya pili ya kambi ya warembo ya Tanzania ambapo mratibu wa masuala ya urembo , Hashimu Lundenga amekutana na warembo thelathini na kutoa tahadhari kwa warembo hao kutojihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu.

    Katika siku hii pamoja na suala la kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu , pia amesisitiza suala la kuheshimu sheria na kuheshimu mkataba walioingia kati ya kamati hiyo na mrembo husika.

    Kambi hii ni ya mwezi mmoja ambapo tamati yake itafikia novemba 5,
    Mrembo atakayepatikana katika shindano hilo atapata fursa ya
    Baadhi ya warembo katika kambi hii mbali na kunyakuwa taji la TANZANIA wengine watanyakuwa taji la vipaji , taji la muonekano mzuri, na taji la mwanamke aliyeng`ara katika michezo.

    Mrembo wa Tanzania atashiriki shindano la dunia litakalofanyika mwezi AUGOST mwakani katika mji wa JAKARTA nchini INDONESIA.

No comments:

Zilizosomwa zaidi