Friday, September 7, 2012

WAZO LANGU. Haya makundi mbalimbali vya muziki maarufu kama "Mduara" yanatoa wapi maadili na ujasiri wa watoto wa kike kukata viono hadharani wakiwa wamevalia Khanga moja? Kama ni uhuru basi wasanii Tanzania wamepewa uhuru uliopitiliza hadi kufikia hatua ya wasanii wenyewe kushindwa kujiheshimu. Hivi kizazi cha leo watoto wanajifunza nini kupitia mchezo kama huo? Ni vizuri basi wasanii walioachiwa huru kuhusika katika muziki huo kufuata maadili, kwani kushindwa kwao kufuata maadili kinachofuata ni kujiabisha wenyewe na taifa kwa ujumla. Pia serikali iliangalie suala hili kwa jicho la pili ili kulinusuru taifa katika wimbi hili zito la "Khanga moja ndembendembe".

No comments:

Zilizosomwa zaidi