Tuesday, September 18, 2012
Askari polisi acheni wizi wakimachomacho. Inasikitisha sana kumkuta askari polisi wa kitengo cha upelelezi kufanya kazi ya askari wa usalama barabarani. Eti unamkuta askari asiyekuwa trafic kuwasumbua waendesha pikipiki (bodaboda) wakati kazi hiyo inatakiwa kufanywa na trafic. Imenisikitisha sana nilipowakuta askari wanne wakiwa umbali wa kilometa 39 kutoka mjini Kasulu mkoani Kigoma wakiwa kwenye barabara ya kuelekea kijiji cha Shunga na Buhoro, wamemsimamisha dereva pikipiki huku wakijifanya kumkagua, kama huo sio ujambazi ninini? Hivi aliyewapa wadhifa huo wa kukamata pikipiki ni nani? Na kama ni hivyo basi wakamate na magari pia sio kuwaonea bodaboda. Hawa polisi badara ya kulinda usalama wetu na mali zetu wamekuwa ni Kero sasa, jambo ambalo linawafanya baadhi ya watu wakiwaona tu, wanaanza kuogopa. Kinachoshangaza ni pale tu wanapokusimamisha, ni lazima uwaachie kiwango flani cha pesa jambo ambalo mi nathubutu kuwaita wao wezi. Polisi jaribuni kubadilika na kila mtu ahusike vizuri katika kitengo alichopo na sio ubabaishaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
JESHI LA wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi kwa kusema kuwa askari wake aliyetoroka jeshini Luteni Kanali Celestine C. Seromba...
-
1.AUSTIN MORRIS A-40 AUSTIN MORRIS A-40 Gari aina ya Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 ...
-
-
INASEMEKANA huyu mwanadada ndiye aliyevunja rekodi ya watu weusi duniani maana maranyingi watu walisubiri atabasamu ili waamin...
-
Msanii maarufu wa Hip...
No comments:
Post a Comment