Picha ikionyesha ukatili dhidi ya waandishi wa habari |
Jumla ya waandishi wa habari 110, wameuawa duniani kote katika kipindi
cha mwaka 2015, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la
maripota wasio na mipaka (RSF) .
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya RSF waandishi wa habari 67 waliuawa wakati
wakitekeleza wajibu wao wa kazi katika kipindi cha mwaka huu, na wengine
43 waliuawa katika mazingira ambayo hayajaeleweka. Waandishi wengine wa
habari 27 wasio na taaluma kamili ya uandishi wa habari na wafanyakazi
wengine 7 kutoka katika vyombo vya habari nao pia waliuawa.
Idadi hiyo kubwa ya vifo vya waandishi wa habari imeelezwa kuchangiwa
zaidi na ukatili unaofanywa dhidi ya waandishi hao wa habari wakati
wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao wa kazi. Hali hii inaashiria
kushindwa kwa hatua za kuwalinda waandishi wa habar.
Chanzo: DW
No comments:
Post a Comment