Mnamo tarehe 17.02.2014 majira ya saa 06:00hrs asubuhi mahabusu aliyefahamika kwa jina la Vumi Elias (30) mkazi wa mtaa wa Maporomoko
Tunduma wilaya ya Momba alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa kituo
cha afya tunduma baada ya kujaribu kujinyonga akiwa ndani ya mahabusu katika
kituo cha polisi Tunduma. Marehemu aliingia katika choo cha mahabusu kilichopo
ndani ya mahabusu hiyo majira ya saa
04:30hrs usiku na kutaka kujinyonga kwa kutumia tambala la kupigia deki.
Marehemu aliokolewa na askari waliokuwa zamu chumba za mashitaka na kukimbizwa
kituo cha afya kwa matibabu akiwa katika hali mbaya na hawezi kuongea baada ya
kupata taarifa kutoka kwa mahabusu wengine walioingia chooni humo. awali mnamo tarehe 14.02.2014 marehemu alikamatwa
kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu. chanzo kinachunguzwa, mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika kituo hicho cha afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Kajala Masanja. Pamoja na kutoa faini ya Sh. milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake wa filamu, Wema Isaac Sepetu, Kajala anat...
-
Matokeo karibu yote yamekwisha kamilika nasi tunamsubiri msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kalenga Bi Pudensiana Kisaka kumtangaza mshindi a...
-
-
-
No comments:
Post a Comment