Godbless Lema |
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ameeleza kushangazwa
na jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe asichukuliwe hatua zaidi kwa madai ya kukinusuru
chama kisisambaratike.
Lema alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kilombero.
Alisema kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kinachowanyima CCM
usingizi, walipaswa kufurahia kusambaratika kwao, lakini cha kushangaza
viongozi wa chama tawala wamekuwa wakiwaasa wasimfukuze Zitto.
“Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Katibu wa Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye wanalia wakitaka tupatane. Mbunge wao wa Kigoma
Mjini, Peter Serukamba naye analia kuwa CHADEMA tumefanya vibaya,
tumrudishe Zitto.
“Sisi tunawauliza tukifanya vibaya ni faida kwao, kwanini wanalia.
CCM wanalalamika CHADEMA hatuna demokrasia, ni chama cha kibabe,
tumemwonea Zitto, kwamba tutapasuka. Hivi tukipasuka wao wataimarika sasa
wanalia nini badala ya kufurahi?” alihoji Lema.
Naye Mwenyekiti wa madiwani wa Jiji la Arusha, Doita Isaya alikemea
tabia ya baadhi ya walimu kuacha kufundisha ipasavyo muda wa kazi ili
baadaye wafanye hivyo kwenye masomo ya ziada ya kujiingizia kipato.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema kipaumbele cha
kwanza cha CHADEMA ni elimu, ndiyo sababu kwa kipindi cha miaka mitatu
walichoongoza halmashauri wameisimamia ipasavyo na kuhakikisha madarasa
51 yanajengwa.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment