Arsenal Wenger amezidi kuchanganyikiwa na tatizo la majeruhi katika
safu yake ya ushambuliaji baada ya kuumia kwa kinda lake Yaya Sanogo na
kuiacha klabu ya Arsenal ikiwa na mshambuliaji mmoja pekee wa kati,Olivier Giroud .
Sanogo mwenye umri wa miaka 21 ambaye mshambuliaji chaguo la pili
katika klabu ya Arsenal ameumia akiwa katika majukutu ya kuitumikia timu
yake ya Taifa ya Ufaransa.
Nyota
huyo anatarajia kupata matibabu ya nguvu makao makuu ya klabu yake,
Colney HQ, Jijini London ili kumuweka sawa kabla ya klabu hiyo kusafiri
kuwafuata Sunderland wikiendi hii, Huku Mesut Ozil akitarajiwa kuanza
kazi rasmi siku hiyo baada ya kusajiliwa kwa ada iliyovunja rekodi ya
Arsenal ya pauni milioni 42.
Majeruhi
hayo yanamaanisha Olivier Giroud amebaki mshambuliaji pekee wa kati
kuelekea mchezo wa jumamosi dhidi ya Sunderland katika dimba la Stadium
of Light.
Sanogo,
aliyesajiliwa majira ya kiangazi mwaka huu akitokeo klabu ya Auxerre ,
alikuwa anatazamwa na Wenger kama mshambulaiji wa baadaye, lakini
kukumbwa na uhaba wa washambuliaji alilazimika kumuweka kikosi cha
kwanza.
Kushindwa kuwasajili
Luis Suarez, Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Karim Benzema na Demba Ba
majira ya kiangazi, kumemuacha Wenger na uhaba mkubwa wa chaguo la
washambuliaji.
Lukas
Podolski angemsaidia Giroud, lakini naye yuko nje kwa miezi mitatu
kutokana na majeruhi ya nyama za oaja, wakati huo Nicklas Bendtner –
anaonekana kutokuwa fiti kabisa.
No comments:
Post a Comment