Kiungo
mchezeshaji mpya wa Arsenal Mesut Ozil hii leo alianza rasmi mazoezi
akiwa na klabu yake mpya baada ya usajili wake wa paundi milioni 42.5
toka Real Madrid .
Ozil
ambaye majuzi aliiongoza Ujerumani kuifungia San Marnio 3-0 huku yeye
mwenyewe akifunga bao moja alionekana mwenye furaha akiwa na wachezaji
wenzie ambao ndio kwanza alikuwa anajenga mazoea nao.
Ozil
aliingia mazoezini akiwa ameambatana na Mjerumani mwenzie Per
Mertesecker pamoja na kocha Arsene Wenger na msaidizi wake Steve Bould
kabla ya kuanza mazoezi hayo ambapo muda mrefu alionekana akiwa karibu
na Metersecker ambaye kwa vyovyote atakuwa akimsaidia kuzoea mazingira
ya London .
Wawili
hao (Ozil na Metesecker) ni wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani na
majuzi walikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa mabao matatu bila
uliowafanya Ujerumani kukaribia kukata tiketi ya michuano ya kombe la
dunia ambapo wote wawili walifunga .
Mesut Ozil anatarajiwa kuanza mchezo wa Arsenal dhidi ya Sunderland utakaopigwa huko Stadium Of Light siku ya jumamosi.
Katika
hatua nyingine baba mzazi wa Mesut Ozil Mustafa Ozil ametishia
kuiburuza klabu ya Real Madrid mahakamani kwa kitendo cha kuchafua jina
la mwanaye .
Baba
huyo amesema kuwa amekerwa na kitendo cha Real kutoa kauli ya kwamba
Ozil aliuzwa kutokana na tabia ya kupenda wanawake na starehe kuliko
kujituma uwanjani.
Mustafa
Ozil alihoji kuwa kama mwanaye alikuwa mpenda satrehe na Real ilimuuza
kwa sababu ya kupenda wanawake kwanini alikuwa akipangwa na makocha wa
timu hiyo kwenye mechi .
Hivi
karibuni jarida la El Mundo lilichapisha makala iliyokuwa inahusu
mienendo ya Oizl ambaye inasemekana alikuwa katika mahusiano ya
kimapenzi na Mrembo toka Venezuela taarifa ambayo iliungwa mkono na Rais
wa Real Florentino Perez.
No comments:
Post a Comment