Zaidi ya watu 39 wameuawa na wengine
150 kujeruhiwa vibaya baada ya watu wenye silaha kuliteka jengo moja lenye maduka la
Westgate,lililopo Jijini Nairobi, Kenya.
Tukio hilo lilitokea jana mchana ambapo watu
waliokuwa wakizungumza lugha ya kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au
Kisomali, kuvamia jengo la ghorofa na kushambulia watu kwa risasi.
Shuhuda mwingine aliyejitambulisha ni mfanyakazi
wa Ubalozi wa Uholanzi jijini Nairobi, Rob Vandijk, alisema tukio hilo
lilitokea wakati akipata chakula cha mchana ndani ya njengo hilo.
Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja baadaye,
Rais Uhuru Kenyatta alithibitisha kuwa zaidi ya watu 39 walikufa katika
shambulizi hilo la kinyama, na wengine 150 kujeruhiwa.
"Vyombo vya usalama vinafanya kila jitihada
kuthibiti eneo hili na kuwakamata waliohusika," alisema Kenyatta,
akiongeza kuwa naye pia amepoteza wanafamilia katika tukio hilo.
Taarifa zingine zilisema kuwa polisi waliwasili eneo la tukio dakika 30 baada ya watu hao kuvamia jengo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kenya, Inspekta Jenerali
David Kimaiyo alisema kwamba polisi walifika katika jengo hilo baada ya
kupata taarifa, ambapo nao walianza kujibizana kwa risasi na magaidi hao
waliokuwa hapo ndani.
Helikopta za polisi zilionekana zikilizunguka jengo hilo kwa juu kuhakikisha hakuna mhalifu yeyote ambaye anaweza kutoroka.
Mashuhuda walisema kwamba walikuwa wakipata
chakula cha mchana jirani na jengo hilo, ghafla wakashuhudia milio wa
risasi kutoka katika eneo hilo.
Baada ya polisi kuingia katika jengo hilo watu
waliokuwa ndani walipata fursa ya kutolewa, huku polisi wengine
wakiendelea kuwatafuta wahalifu hao.
Al-Shabab Yazungumza
Wakati shambulizi likiendelea jana jioni,
wanamgambo wa kikundi cha Kiislamu cha Al-Shabab walivyambia vyombo vya
habari kupitia Twitter kuwa wamehusika na tukio hilo.
Wanamgambo hao waliongeza kuwa wamefanikiwa kuua
watu wengi kuliko idadi inayotajwa na serikali ya Kenya, huku wakibeza
jitihada za uokoaji.
"Tulishaionya serikali ya Kenya kuwa dhahama itaikumba kamaisipoondoa vikosi vyake kutoka Somalia,” Al-Shabab waliandika kupitia akaunti yao ya Twitter inayoitwa @HSM_Press.
"Tulishaionya serikali ya Kenya kuwa dhahama itaikumba kamaisipoondoa vikosi vyake kutoka Somalia,” Al-Shabab waliandika kupitia akaunti yao ya Twitter inayoitwa @HSM_Press.
Kutokana na malalamiko kutoka kwa waathirika wa tukio na vyombo mbalimbali vya usalama, FastCompany inaripoti kuwa Twitter ililazimika kuifunga akaunti hiyo jana usiku.
No comments:
Post a Comment