Saturday, August 10, 2013

WYNE ROONEY HATARINI KUIKOSA NAFASI TIMU YA TAIFA....

Roy Hodgson
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hudson amemuonya mshambuliaji wa Mancheter United Wyne Rooney kuwa kunahatari ya yeye kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa endopo hatapata nafasi ya kupangwa kikosi cha kwanza katika club yake.
Rooney amekuwa akihofia nafasi yake ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Man United kutokana na meneja mpya wa mabingwa hao wa England David Moyes kumpa kipaumbele mshambuliaji Robin Van Persie, huku mabingwa hao wameshakataa ofa mbili kutoka kwa wapinzani wao Chelsea kutaka kumsajili Rooney.
Wyne Rooney
Hudson amesema itakua ngumu sana kuendelea kumchagua mchezaji wa miaka 27 kama hapati nafasi kucheza mara kwa mara kwenye club yake.
Jina la Rooney limetajwa kwenye kikosi cha England kinachojiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Scotland itakayopigwa katika uwanja wa Wembley Jumatano ingawa ameikosa micheza yote ya kabla ya msimu ambayo Man United imecheza kwenye tua yao huko Asia kutokana na majeraha aliyoyapata mwanzoni mwa tua hiyo ya Man United.
By Mligo G

No comments: