Sunday, August 25, 2013

HILI NDILO KANISA LA KKT LILILOLIPULIWA MAENEO YA SEGEREA, JIJINI DAR.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) ushirika wa Segerea limenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kutupa chupa iliyodhaniwa kuwa na mafuta ya taa au ya petroli na kulipuka ndani ya kanisa na kuunguza baadhi ya vitu vilivyowemo katika madhabahu ya kanisa pamoja na gari lililokuwa nje ya kanisa hilo majira ya saa 8 usiku
wa kuamkia jana.
 
Akielezea tukio hilo mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Segerea Bwana Noha Kipingu, amesema tukio limetokea majira ya saa 8 za usiku ,wakati baadhi ya waumini wakiwa ndani ya kanisa katika maombezi ya yaliyoanza saa 4 usiku kwa ajili ya mkutano uliokuwa unaotarajiwa kufanyika jumapili ya leo agosti 25.
Akielezea msimamo wa kanisa KKKT usharika wa Segerea kuhusu tukio hilo, licha ya kusisitiza linachukuliwa kama sehemu ya matukio mengine ya ulipuaji wa makanisa yanayoendelea,amesema kwa mujibu wa maelezo ya mlinzi wa kanisa ameona watu wanne waliotega chupa na kulipua kwenye gari la kanisa pamoja na kurusha chupa nyingine ndani na kisha kukimbia.
Baadhi ya waumini walionusurika katika tukio hilo wamesema wamesikia mshindo mkubwa wa kitu kinachofanana na bomu katika madhabau ya kanisa hilo wakati wakiwa wamesimama mbele ya kanisa hilo na kisha moto ukaanza kuunguza madhabau hali iliyowafanya kukimbia na kisha kurudi ndani kwa ajili ya kuzima moto huo.

No comments:

Zilizosomwa zaidi