Abiria
wapatao 60 waliokuwa wanasafiri siku ya jana na basi la Turu linalofanya safari zake
kati ya mkoa wa Singida na Haidom mkoani Manyara, walilazimishwa
kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 )
wa vijiji vitatu, na kisha kulichoma moto basi hilo.
Wananchi hao ni wa vijiji vya Singa,
Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria
wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu
kubwa.
Hii ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.