Monday, May 27, 2013

HII NI KUTOKA KWA BLOG MOJA HIVI: MIPANGO YA KUMNG'OA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI DK KAWAMBWA IMEKAMILIKA

WAKATI Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), ikitarajia kutangaza matokeo mapya ya kidato cha nne, baada ya kufanya marekebisho ya alama za viwango vya ufaulu, njama za kukwamisha Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafun
zo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa inaadaliwa.
Habari zilizonaswa na Habarimpya.com zinadai kwamba, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejipanga kukwamisha hotuba ya Wizara hiyo, kwa madai kwamba Waziri huyo ameshindwa kusimamia sekta ya Elimu.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM mjini Dodoma zinadai kwamba, Wabunge hao wamepania kukwamisha hotuba hiyo na kumtaka Waziri huyo ajiuzuru ili kukisafisha Chama hicho kutokana na aibu ya mkanganyiko wa kufeli kwa Wanafunzi mwaka huu.
"Hotuba ya Wizara ya Eilimu haiwezi kupitishwa kirahisi kama Kawambwa hata jiuzuru, hatuwezi kuendelea kuwa na mawaziri wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo katika setka zao, kitendo cha mawaziri hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ndiyo inayochangia kuharibu Chama"kilisema chanzo hicho kwa masharti ya kutotajwa majina yake na kuongeza.
"Huu mpango unaendelea kusukwa na wabunge wa CCM waliopania kurudisha heshma ya Chama, lakizima tuanzie ndani kuwajibishana wenywe kabla ya wapinzani kuanza, kwani tukishindwa sisi watatumia udhaifu wetu kuwashawishi wananchi na hatimaye watazidi kuichukia Serikali".  
Wakati Waziri Dk Kawambwa akiandaliwa mazingira ya kung'olewa, Necta inatarajia kutangaza matokeo yaliyoongeza kiwango  cha  ufaulu kufikia asilimia kati ya 54 na 57, wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Kutangazwa kwa matokeo hayo pia yamesababisha hotuba ya Wizara ya Elimu kuondolewa katika ratiba ya kawaida na sasa italetwa bungeni Juni 3.  
Taarifa zinaeleza kuwa, kusogezwa mbele kwa hotuba hiyo kunatokana na mipango ya Serikali ambayo inatafuta namna ya kukamilisha mchakato wa matokeo ya kidato cha nne ili kuipa mteremko hotuba ya Waziri wa Elimu.

No comments:

Zilizosomwa zaidi