Friday, March 15, 2013

ZIMBABWE KUPIGA KURA YA KATIBA MPYA LEO.


wapiga kura katika foleni

Zimbabwe inapigia kura ya maoni kielelezo cha katiba 
hii leo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi ufanyike 
nchini humo uliokumbwa na utata mwaka wa 2008.
Hata hivyo malalamiko yametolewa kuwa huenda nchi hio 
haijajiandaa vilivyo kutokana na ukosefu wa fedha za 
kutosha na wachunguzi wanadai kuwa wamefungiwa nje
ya shughuli hiyo.
Mugabe na Tsvangirai

Lakini kwa mara ya kwanza inaonekana kuwa hakuna
 Utata uliojitokeza katika kura hii. Chama chake rais 
Robert Mugabe ZANU - PF na kile cha upinzani 
ambacho sasa kiko katika serikali ya muungano MDC, 
vyote vinaunga mkono kielelezo hicho cha katiba.
Katiba hiyo inapendekeza kuhifadhiwa nafasi ya rais 
mwenye nguvu nyingi serikalini na hii inampa rais Mugabe 
uwezo wa kusalia madarakani kwa miaka kumi zaidi.

Hata hivyo kura hii ya maoni haijawachangamsha sana 
wananchi wa Zimbabwe huku raia wengi wakionekana 
kulenga zaidi uchagzui mkuu unaopangwa kufayika miezi chache zijazo.
Katiba mpya inatazamiwa kunyoosha njia ya 
kufanyika uchaguzi huo mkuu japo kuna wasiwasi 
kwa machafuko zaidi kutokea nchini humo.

No comments:

Zilizosomwa zaidi