Uongozi
wa klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji leo
umewatambulisha rasmi wajumbe wa Bodi ya Baraza la Wadhamiini ambao
watafanya kazi zote ambazo zitahusiana na klabu ya Yanga (Mali na
Ufilisi) kufuatiwa kupitishwa na wanachama katika mkutano mkuu.
Yanga ilifanya mkutano mkuu mwezi Januari 20, 2013 mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi Oysterbay ambao wanachama
wa klabu walilridhia kuwaongezea tena mda Mama Karume na Francis Kifukwe
amabao awali walikua wamemaliza mda wao wa miaka miwili.
Katika
mkutano huo wanachama waliridhia kwa mwenyekiti kuongeza idadi ya
wajumbe wa bodi ya wadhamini kutoka wawili waliokuwepo na kufikia
wajumbe saba, ambapo kwa sasa klabu itakua na wajumbe wanne na kamati ya
utendaji itapata fursa ya kuongeza wengine watau ili kufikia idadi ya
wajumbe saba.
Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya
klabu ya Yanga, Manji amesema uteuzi huo wa bodi ya wadhamini
umezingatia wasifu wa wajumbe hao ambao wamewahi kufanya kazi katika
sekta mbali mbali ndani na nje ya nchi.
Klabu ya Yanga awali ilikua na wajumbe wawili wa Bodi ya wadhamini ambao ni Mama Fatma Karume na Injinia Francis Kifukwe.
Kwa
sasa bodi ya wadhamini itakua na wajumbe wa wanne (4) ambao ni Mama
Fatma Karume, Francis Kifukwe, na wajumbe wapya waliotambulishwa leo ni
Balozi Ami Mpungwe na Kaptain George Mkuchika.
Akitoa wasifu wa
wajumbe hao, Manji alisemaBalozi Amir Mpungwe amekua ni kiongozi wa
serikali kwa nyadhifa mbali mbali kwa miaka kadhaa, amekua Balozi wa
kwanza Tanzania nchini Afrika Kusini mara baada ya nchi hiyo kupata
uhuru na kwa sasa anafanya shughuli zake binafsi.
Kaptain George
Mkuchika ni waziri wa nchi ofisi ya waziri utawala bora pia amekua
kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbalimbali na hata katika chama chake
amekua kiongozi makini kwa muda mrefu.
Aidha kuhusu Mama Fatma
Karume na Mzee Kifukwe mwenyekiti amesema wanafahamika kwa kazi zao
walizozifnya kwa maendeleo ya klabu ya Yanga hali iliyopelekea mkutano
mkuu wa wanachama kuwaongezea muda tena wa miaka miwili.
Mara
baada ya kutambulishwa rasmi na kupewa katiba za Yanga mwenyekiti
alitumia fursa hiyo kuwazungusha wajumbe kuona majengo na mali za klabu
kabla ya kupiga picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment