Wednesday, October 17, 2012

MGAMBO MBIO KALI, SIMBA, AZAM KIMYA.

MGAMBO Shooting wameendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuichapa Toto African kwa mabao 2-0, huku Simba  ikitoka sare na Kagera Sugar huku Azam  nayo ikitoka sare na Tanzania Prisons.
Kwa ushindi huo umeifanya Mgambo Shooting kupanda hadi nafasi ya 8 ikiwa na pointi 9 katika msimamo huo unaoongozwa na Simba wenye pointi 18 wakifuatiwa na Azam (17) na JKT Oljoro (13).
Mgambo Shooting iliyopanda daraja msimu huu imeweka rekodi ya kushinda mechi yake ya tatu mfululizo baada ya kuanza ligi kwa kusuasua ikiwa imepoteza michezo mitano kabla ya kushinda dhidi ya Polisi Moro na Mtibwa Sugar.

Mgambo Shooting wakiwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani walipata bao la kuongoza katika dakika ya 58 kupitia kwa Full Maganga aliyeunganisha kwa kichwa pasi iliyopigwa na Yasin Awadhi kabla ya Issa Kanduru kupachika bao la pili katika dakika ya 62 akiunganisha kona iliyopigwa na Salum Kipanga na kuichapa Toto African 2-0.

Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wameendelea kusuasua baada ya kupoteza pointi nne katika michezo miwili mfululizo kufutia sare yao dhidi ya Coastal Union na Kagera Sugar.

No comments:

Zilizosomwa zaidi